Aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi, Roger Lumbala (67), amehukumiwa na Mahakama ya Paris kifungo cha miaka 30 jela kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu uliotekelezwa wakati wa Vita vya Pili vya DR Congo. Mahakama imesema Lumbala aliagiza au alishiriki kusaidia vitendo vya mauaji, ubakaji, utumwa wa kingono, kazi za kulazimishwa na uporaji vilivyotekelezwa kati ya mwaka 2002 na 2003, alipokuwa kiongozi wa kundi la waasi la RCD-N. Waendesha mashtaka waliiomba Mahakama kuwa Lumbala, ahukumiwe kifungo cha maisha, lakini mahakama iliamua kumpa miaka 30. Hata hivyo, kesi hiyo imesifiwa na watetezi wa haki za binadamu duniani kama hatua muhimu […] The post Aliyekuwa kiongozi wa waasi DRC ahukumiwa miaka 30 jela appeared first on SwahiliTimes .