Rais Mwinyi ateua wakuu wa Mikoa, Manaibu Katibu Wakuu

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi amefanya teuzi tano huku kati ya hizo tatu zikiwa ni nafasi za wakuu wa mikoa na mbili manaibu katibu wakuu. Katika taarifa kwa vyombo vya habari imeelezwa kuwa viongozi hao wataapishwa kesho Jumatano Desemba 17, 2025 saa 8:00 mchana Ikulu Zanzibar. Written by Janeth Jovin