Maafisa watatu wa uhamiaji wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji

Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa maafisa watatu wa Uhamiaji; Fredrick Kyomo, Joachim Trathizius na Mabruki Hatibu, kwa kosa la kumuua Enos Elias, mkazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, ambaye walidhania kuwa si raia wa Tanzania. Hukumu hiyo imetolewa Desemba 15, 2025, na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Augustine Rwizile, ambapo amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani umeonesha bila shaka yoyote kuwa hakuna mtu mwingine au kundi lolote lililohusika katika mauaji hayo isipokuwa maafisa hao watatu. “Kwa kuzingatia ushahidi unaoonesha namna walivyomkamata, kumshambulia, na baadaye kumpeleka mahali pasipojulikana ambako alikutwa amefariki, vitendo hivyo vinatosha kuthibitisha kuwa washtakiwa […] The post Maafisa watatu wa uhamiaji wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji appeared first on SwahiliTimes .