Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeingia makubaliano ya uendeshaji wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center (ALMC) kwa kipindi cha miaka 20 ijayo, hatua itakayoimarisha huduma za matibabu ya kibingwa ya magonjwa ya moyo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.