Mchakato upangaji majaji kesi za uchaguzi Zanzibar kuanza Desemba 23

Mchakato wa upangaji wa majaji watakaosikiliza kesi za kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, katika majimbo manane Zanzibar, sasa unatarajiwa kuanza Desemba 23, 2025 baada ya kukamilika kwa taratibu za ubadilishanaji nyaraka za kesi hizo.