Madumu 23,755 ya mafuta ya magendo yakamatwa, wafanyabiashara walia urasimu
Wakati Serikali ikikamata madumu 23,755 ya mafuta ya kula yaliyoingizwa nchini kinyume na taratibu, wananchi wamepaza sauti zao wakitaka watumishi waliopo bandari ndogo ya Kunduchi, kuangaliwa kwa kile wanachodai wamekuwa wakikwamisha biashara.