Serikali: Tanzania na Marekani zitaendeleza mazungumzo kuhusu udhibiti wa viza

Serikali imesema itaendeleza mazungumzo ya kidiplomasia na Serikali ya Marekani yanayolenga kupata muafaka kuhusu uamuzi wa kuiweka Tanzania katika kundi la nchi 15 ambazo zimewekewa udhibiti wa viza kuingia nchini humo. Uamuzi huo uliotangazwa Desemba 16, 2025 na Rais wa Marekani, Donald Trump umehusisha nchi 15 ambazo ni Angola, Antigua na Barbuda, Benin, Ivory Coast, Dominica, Gabon, Gambia, Malawi, Mauritania, Nigeria, Senegal, Tonga, Zambia na Zimbabwe. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi imesema udhibiti huo umetokana na kuwepo kwa idadi ya baadhi ya raia wa Tanzania kuzidisha muda wa kukaa Marekani kinyume na masharti ya viza. […] The post Serikali: Tanzania na Marekani zitaendeleza mazungumzo kuhusu udhibiti wa viza appeared first on SwahiliTimes .