Rais Mwinyi asisitiza kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na TRA kuimarisha ukusanyaji mapato

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika juhudi za kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo, hususan katika maeneo muhimu ya ukusanyaji wa mapato. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Desemba 17, 2025, alipokutana na Kamishna Mkuu wa TRA, Yussuf …