Polisi waanza uchunguzi waombolezaji kuchoma magari yaliyosafirisha mwili wa marehemu

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limesema linafanya uchunguzi wa tukio la kuchoma na kuharibu magari mawili katika Wilaya ya Mvomero yaliyokuwa yakisafirisha mwili wa marehemu. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema tukio hilo limetokea Desemba 17, 2025 katika Kata ya Diongonya, Tarafa ya Turiani wilayani Mvomero, ambapo gari yenye namba T. 214 EJU aina ya Mazda CX-5 na T. 350 DCH aina ya Toyota Noah yalichomwa moto na kuharibika na waombolezaji wa msiba. “Magari hayo yalitumika kusafirisha mwili wa marehemu Mwanahasan Hamis (18) mfanyakazi wa kazi za ndani mkazi wa Turiani, aliyefariki kwa maradhi jijini Dar es Salaam kisha […] The post Polisi waanza uchunguzi waombolezaji kuchoma magari yaliyosafirisha mwili wa marehemu appeared first on SwahiliTimes .