Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amewaagiza viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuendelea kuchukua hatua kali zaidi za kisheria dhidi ya waajiri wa sekta binafsi wanaoshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.