Wanafunzi 15,003 waliokatisha masomo warejeshwa kwenye mfumo wa elimu

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imesema, kwa kipindi cha miaka mitano, wanafunzi 15,003 waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito, wamesajiliwa kujiunga na programu za elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi wa elimu.