Polisi Morogoro wachunguza kifo cha msichana, magari yakichomwa moto
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tukio la kuchomwa moto na kuharibiwa kwa magari mawili katika Wilaya ya Mvomero, tukio lililotokea Desemba 17, 2025.