SWALI: Shikamoo Shangazi? Nimegundua kuwa binti yangu mwenye umri wa miaka 17 amepachikwa mimba na mwanaume nisiyemjua. Hii ina maana kwamba hataendelea na masomo yake kama kawaida mwaka ujao. Najihisi nimevunjika moyo hata sijui nianzie wapi. Nipe ushauri. Jibu : Si kweli kwamba hawezi kuendelea na masomo yake mwaka ujao. Akijifungua anaweza kuendelea na masomo. Hasira hazikutasaidia kutatua tatizo hili. Unafaa kusimama na mtoto wako kwa vyovyote vile. Mpe matumaini katika maisha yake ya baadaye. Mpe ushauri ufaao na mwelekeo bora kwamba asikate tamaa ila atasoma kama wenzake hapo baadaye. Makosa yamefanyika hivyo, kabiliana nayo bila kumkaripia. IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO