‘Wananchi bado hawajaelewa kikamilifu huduma za ZHSF’

Meneja wa Kitengo cha Uhusiano wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF), Asha Kassim Biwi amesema kuwa bado kuna changamoto kwa baadhi ya wananchi kutoelewa kikamilifu huduma zinazotolewa na mfuko huo, hali inayosababisha upotoshaji na matumizi duni ya fursa zilizopo.