Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Festo Lulandala amepiga marufuku shughuli za usafishaji wa mashamba mapya kwa ajili ya kilimo Kata ya Langai, hatua inayolenga kutoa fursa ya kuchunguza na kusuluhisha migogoro ya ardhi inayolikumba eneo hilo.