Wapagazi 30,000 waungana, waanzisha TAP kutetea haki zao

Zaidi ya wapagazi 30,000 kutoka vyama vinne nchini wameungana na kuunda umoja wao uitwao Tanzania Association of Porters (TAP), kwa lengo la kuimarisha mshikamano miongoni mwao na kuweka mfumo wa pamoja wa kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika sekta ya utalii.