Serikali ya Rwanda imefunga zaidi ya makanisa 10,000 kwa kushindwa kutimiza masharti ya sheria ya mwaka 2018 inayodhibiti maeneo ya ibada nchini humo. Sheria hiyo iliweka masharti mapya kuhusu afya, usalama na uwazi wa kifedha, na pia inamtaka kila mhubiri kuwa na mafunzo ya theolojia. Akizungumza na waandishi wa habari, Rais Paul Kagame amesema haoni mchango mkubwa wa baadhi ya makanisa katika kutatua changamoto za dunia kama vile vita na ukosefu wa ajira. Amesema badala ya kusaidia jamii, yapo makanisa yanayotumiwa kama njia ya kujinufaisha binafsi. Agosti mwaka huu zaidi ya makanisa 4,000 yalifungwa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya […] The post Rwanda yafunga makanisa zaidi ya 10,000 appeared first on SwahiliTimes .