Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imeiamuru kampuni ya UDA Rapid Transit (UDART) kumlipa Frank Zebaza fidia ya shilingi milioni 88.8, baada ya kugongwa na basi la Mwendokasi. Katika hukumu iliyotolewa Desemba 19, 2025, mahakama pia imebaini kuwa dereva wa basi hilo, Hafidhi Ally, alikuwa akiendesha kwa uzembe na akamwamuru kumlipa mlalamikaji shilingi milioni 10 binafsi. Uamuzi huo umetokana na kesi ya madai iliyofunguliwa na Zebaza dhidi ya UDART, dereva wa basi, Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Awali, Zebaza alikuwa akiomba fidia ya jumla ya TZS milioni 600 kwa […] The post Aliyegongwa na Mwendokasi kulipwa milioni 88 appeared first on SwahiliTimes .