Kongani ya viwanda Kahama kuwa kitovu cha uzalishaji, usambazaji ukanda wa SADC

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema kongani maalumu ya viwanda inayojengwa katika eneo lililokuwa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, inatarajiwa kuwa kitovu kikubwa cha uzalishaji na utoaji wa bidhaa na huduma kwa migodi iliyopo kusini mwa Jangwa la Sahara ndani ya ukanda wa SADC.