NAOT kushirikisha wadau ripoti za ukaguzi

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) imesema itaendelea kushirikisha wadau wazielewe ripoti za ukaguzi na kuchangia katika kuimarisha uwajibikaji wa matumizi ya rasilimali za umma. Mchumi Mwandamizi wa NAOT, Emanuel Lazaro amesema hayo alipowasilisha mada kuhusu njia na aina za ukaguzi wakati wa mafunzo ya ukaguzi kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro . The post NAOT kushirikisha wadau ripoti za ukaguzi first appeared on HabariLeo .