TANZANIA imeihakikishia Malawi kuwa ipo tayari kuendelea kushirikiana katika biashara ya mahindi. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Dk Stephen Nindi amesema hayo baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Malawi, Erica Maganga jijini Lilongwe, Malawi. The post Tanzania kuendelea kuuza mahindi Malawi first appeared on HabariLeo .