Serikali imewataka wamiliki wote wa maeneo ya kazi nchini ambao bado hawajayasajili maeneo yao na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuhakikisha wanasajili maeneo hayo ndani ya siku 90 kuanzia Januari 2026, hatua inayolenga kuimarisha usalama na afya kwa wafanyakazi nchini. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu …