Jeshi la Polisi mkoani Pwani limekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu gari la Jeshi la Polisi kumgonga mwananchi eneo la Korogwe, Kibaha na kusababisha kifo chake, likiwataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa pasipo kuwa na uthibitisho wa mamlaka husika. Polisi wameeleza kuwa Desemba 19, 2025 majira ya saa 2:00 usiku eneo la Kongowe barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam gari ambalo halikutambulika namba za usajili lilimgonga mwanamke aliyefahamika kwa jina la Pendo Mashauri (20), mkulima na mkazi wa Kongowe na kumsababishia majeraha. “Hata hivyo ajali hiyo haikuripotiwa kwa wakati katika kituo chochote cha Polisi badala yake ilipelekwa taarifa […] The post Polisi wakanusha kumgonga mwananchi na kumsababishia kifo Kibaha appeared first on SwahiliTimes .