Masauni: Mitazamo potofu ya vijana inahatarisha Muungano, waelimishwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni, amesema Muungano wa Tanzania unaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali, akionya kuwa iwapo vijana hawatapewa elimu sahihi kuhusu misingi ya Muungano huo, upo hatarini kuvunjika.