Wahariri wahimizwa kulinda amani na masilahi ya Taifa
Mwanadiplomasia Mwandamizi, Omar Mjenga, amewataka wahariri wa vyombo vya habari kuwa chimbuko la hoja na mijadala mipana kuhusu umuhimu wa kulinda amani na masilahi ya Taifa, hasa ya jamii inapotofautiana kimtazamo.