Ajira kwa watoto yashamiri mnadani Maswa

Licha ya Serikali kupiga marufuku ajira kwa watoto wadogo na kuweka sheria kali za kulinda haki zao, vitendo vya kuwatumikisha bado vinaendelea kwa kasi katika mnada mjini Maswa, mkoani Simiyu, hali inayozua maswali kuhusu utekelezaji wa sheria na uwajibikaji wake.