Sh485 milioni zanufaisha vikundi 15

Mbunge wa Mbeya Vijijini, Patali Shida amekabidhi mkopo wa Sh485 milioni uliotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwa vikundi 15 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.