Meneja Mauzo wa Vodacom wilaya ya Hai, Gallus Massama (kulia), akikabidhi kapu Vodacom kwa ajili ya sikukuu kwa mkazi wa Njoro mjini Moshi, Asia Iddy Kasimu (kushoto) ikiwa ni muendelezo wa kampeni kugawa makapu kwa wateja katika msimu huu wa sikukuu. Kampeni hiyo imeendelea katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Hafla hii imeandaliwa kwa lengo la kusherehekea pamoja na wateja, sambamba na kuhitimisha maadhimisho ya miaka 25 ya Vodacom ya utendaji kazi nchini, na limefanyika mjini Moshi, mkoani kilimanjaro jana. The post Vodacom yagawa makapu ya sikukuu kwa wateja wake Moshi appeared first on SwahiliTimes .