Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu ya umoja na amani, kupinga chuki, migawanyiko na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mshikamano waTaifa. Ametoa wito huo leo Desemba 25, 2025 aliposhiriki ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri la Azani Front jijini Dar es Salaam. “Manufaa ya amani ni makubwa; huleta maendeleo ya kiuchumi, huimarisha ustawi wa jamii, na huwezesha kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa,” amesema. Amesema Serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda amani na usalama wa nchi pamoja na kuwajenga Watanzania […] The post Viongozi wa dini wahimizwa kuendelea kufundisha kuhusu umoja na amani appeared first on SwahiliTimes .