Maafisa 2 wauawa Moscow karibu na alikouawa jenerali wa Urusi

WATU watatu wakiwemo maafisa wa polisi, wameuawa baada ya bomu kulipuka jijini Moscow karibu na eneo ambalo jenerali mkuu wa jeshi la Urusi aliuawa siku mbili zilizopita. Urusi imesema mauaji ya jenerali huyo yalipangwa na idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine. Tukio hilo ni sehemu ya msururu wa mashambulio yaliyolenga maafisa wa kijeshi wa Urusi na watu mashuhuri wanaounga mkono vita dhidi ya Ukraine. Kamati ya Kitaifa ya Upelelezi ya Urusi ilisema maafisa hao wawili waliuawa walipomkaribia mtu ambaye alionekana kuwa na ‘tatizo’ fulani. “Kulikuwa na mlipuko,” alisema mkazi wa eneo hilo kwa jina Alexander alipokuwa akizungumza na televisheni ya Reuters. “Ilikuwa sauti kubwa sana, kama mlipuko wa gari uliotokea siku chache zilizopita.”