MSWADA wa Fedha wa 2024 ulipokataliwa na Rais William Ruto baada ya maandamano yaliyoongozwa na vijana wa Gen Z, serikali ilijua ingekabiliwa na mwaka mgumu kifedha. Mswada wa Fedha uliokataliwa ulitarajiwa kukusanya nyongeza ya Sh346 bilioni katika mapato ya serikali. Kilele cha maandamano hayo kiliishia kwa waandamanaji kuvunja majengo ya bunge mnamo Juni 25, mwaka huo. Msururu wa harakati ulifuatia kwa kuwa serikali haikuwa na budi kuziba pengo kwa kuhakikisha huduma zote muhimu zinaendelea pasipo kukatizwa. Majukumu ya mikopo iliyochukuliwa na serikali yalikuwa sharti yatimizwe kwa wakati. Akitupilia mbali mswada huo uliokuwa umepitishwa na Bunge kwa njia tatanishi na kukaidi shinikizo la umma, Rais Ruto aliitisha kupunguza matumizi ya pesa serikalini ili kufidia upungufu uliotarajiwa kwenye mapato ikiwemo migao ya fedha zilizotengewa serikali. Notisi ilisambazwa kutoka Hazina Kuu kwa wahasibu wote wakiagizwa kupunguza matumizi hadi asilimia 15 ya bajeti, hadi bajeti ndogo itakapobuniwa. Wakosoaji hata hivyo, walizua maswali kuhusu utekelezaji wa amri hiyo na mikakati mingineyo ya kupunguza matumizi. Katika mahojiano na Taifa Dijitali , Waziri wa Fedha John Mbadi alitaja mwaka huo kama “uliokuwa mgumu”. “Ulikuwa mgumu. Mikopo kadhaa ilikuwa inatimiza muda unaostahili kukamilisha kulipa, tulikuwa na Mikataba ya Malipo (CBA) iliyokuwa pia inafikisha muda wake, ni sharti tungelipa mishahara ya watumishi wa umma kama kawaida na sisi kama serikali tulilazimika kudhibiti gharama ghali ya maisha,” alisema Bw Mbadi. “Yote haya halihitajika kufanywa pasipo kuongeza hata senti kupitia ushuru kwa sababu umma ulitiwasumu kupinga chochote kinachoitwa ushuru kutoka kwa serikali.” Bw Mbadi, aliyerithi hazina kuu iliyokuwa imesakamwa na lindi la malipo ya madeni huku kukiwa na mapato ya chini, alisema walilazimika ilikuwa sharti wakabiliane na hali zote ibuka na kudumisha kiwango cha uchumi, maamuzi machungu yalilazimika kufanywa na ilikuwa shartoi yafanywe kwa dharura. “Tulianza kupunguza matumizi kwa mambo yasiyo muhimu serikalini na kuanza kupima matumizi yetu katika asasi zote za serikali, hatua hii ilituokolea mabilioni kadhaa tuliyotumiwa katika nyanja nyingine zilizosukumwa zaidi,” alisema. Ili kukabiliana na deni la Eurobond ambalo Mbadi ealihofia kwamba serikali ilikuwa karibu kukosa kulipwa mwaka jana, Waziri alisema serikali ililazimika kuitisha Eurobond nyingine ili kuzuia tishio la kufeli kulipa. Mapato ya juu ya ushuru katika Mswada wa Fedha wa 2024 yalidhamiriwa kupunguza mapungufu kwenye bajeti ya serikali hivyo kupunguzia taifa mzigo wa deni. Waziri alitaja vipengee kama vinavyolenga kupunguza matumizi ya ushuru na kurefusha muda wa msamaha wa ushuru kuwa baadhi ya vipengee vipya katika Mswada wa Fedha uliokataliwa ambavyo Mbadi anasema vilikuwa bora kwa uchumi. Kulingana na Waziri, kutokana na serikali kuingilia katika uchimbaji madini,sekta hiyo imekuwa pakubwa kutoka asilimia 2.9 hadi asilimia tano. Alisema serikali tayari imelipa malimbikizi ya madeni ya jumla ya Sh70 bilioni huku kiasi kilichosalia kikielekea kulipwa kikamilifu. Mpangilio mpya wa bajeti bila pesa unahitaji idara za serikali kuthibitisha sababu ya matumizi yote kwa kila mwaka mpya wa kifedha kinyume na kupanga bajeti kwa kutumia migao ya awali. Mageuzi hayo yananuiwa kuimarisha uwazi, kuboresha utendakazi wa matumizi na kuhakikisha fedha za umma zinaelekezwa katika maeneo yanayostahili kupatiwa kipaumbele.