Mvua zakwamisha safari za treni za SGR

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limepata changamoto kwenye mfumo wa umeme karibu na Stesheni ya Ruvu mkoani Pwani, hali iliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini. Akizungumza na Swahili Times, Afisa Habari wa TRC, Fred Mwanjala amesema kwa sasa mafundi wako eneo la tukio kuhakikisha wanarejesha miundombinu ili huduma za usafiri zirejee kama kawaida. “Napenda kuwaomba radhi abiria wetu kwa changamoto iliyojitokeza, hilo ni suala ambalo huwezi kuliepuka ni suala la kiufundi,” amesema Mwanjala. Shirika hilo limewashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu nyakati zote. The post Mvua zakwamisha safari za treni za SGR appeared first on SwahiliTimes .