Abiria SGR wasota stesheni, TRC yaeleza sababu

Wakati abiria wa treni ya kisasa (SGR) wakilalamika kusota kwa muda stesheni bila safari kuanza, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeeleza hali hiyo imesababishwa na changamoto za kiufundi zilizotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.