Pasta ajiuzulu baada ya Gen Z kususia harusi mwaka mzima

ENILOPOLIS, BRAZILI Pasta wa kanisa moja hapa alijiuzulu baada ya washirika vijana kukosa kufunga harusi mwaka mzima. Vijana hao walisema kiongozi huyo hakutoa mfano mwema wa maisha ya ndoa na uwajibikaji waliotarajia. Taarifa kutoka kwa wazee wa kanisa ilisema kuwa hatua hiyo iliibua mjadala mpana kuhusu maadili ya uongozi wa kidini. Baada ya mashauriano marefu, baraza simamizi la kanisa lilikubali uamuzi wa pasta huyo kujiuzulu na kusema alikuwa na uhuru wa kuendelea kuwa mshirika wa kawaida japo inasemekana anapanga kuhamia jiji tofauti.