Uchaguzi mdogo jimbo la Fuoni kesho bila ACT - Wazalendo

Uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Fuoni, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, unafanyika kesho, Jumanne Desemba 30, 2025, kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Ali Mwinyi.