Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewataka wamiliki wa viwanja 6,560 vilivyoko maeneo ya Mtumba na Kikombo kulipia viwanja vyao ndani ya siku 21, ikisisitiza kuwa kushindwa kufanya hivyo kutasababisha viwanja hivyo kuhamishiwa kwa watu wengine wenye uhitaji.