Kesi ya 'vigogo wa Kigamboni' wanaodai kuchepusha fedha za Tamisemi, kuunguruma Januari 13

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Januari 13, 2026 kuanza kusikiliza ushahidi wa upande w Jamhuri katika kesi ya kuchepusha fedha na kuisababishia Wizara ya Tamisemi hasara ya Sh165 milioni, inayowakabili washtakiwa 13, wakiwemo wakuu wa idara wa manispaa ya Kigamboni.