MAMLAKA ya Vitambulisho ya Taifa (NIDA) imezindua namba ya kutuma ujumbe mfupi wa kufahamu namba ya utambulisho ya mwombaji wa kitambulisho itakayowezesha wananchi kufahamu namba zao za vitambulisho bila kufika ofisini na kupunguza msongamano wa kupata vitambulisho vya taifa. Imesema namba hiyo itawezesha waombaji wa vitambulisho hivyo kufuatilia hali ya maombi yao hatua kwa hatua … The post Namba ya NIDA sasa kupatikana kwa ujumbe mfupi first appeared on HabariLeo .