Mbinu zake mpya chumbani zanifanya nishuku anafunzwa na mwanaume mwingine; nishauri

Mpenzi wangu wa miaka miwili ameanza kuleta mbinu za kiajabu kitandani, suala linalonifanya kudhani kwamba ananijifunza kwa wanaume wengine huko nje. Nishauri! Mabadiliko ya mwenendo wa kimapenzi peke yake sio ushahidi wa usaliti, kwani watu hukua, hujifunza au hujaribu kuimarisha ukaribu wao. Badala ya kuwaza mabaya kimya kimya, kaa naye chini umzungumzie kwa uwazi na heshima kuhusu hisia zako na hofu zako, bila lawama. Mawasiliano ya wazi huondoa mashaka mengi kuliko upelelezi, na kama kuna tatizo, ukweli hujitokeza kupitia mazungumzo. Mume alibagua mtoto aliyenioa naye kwa kutompa zawadi Krismasi Mume wangu aliwanunulia watoto wetu nguo za Krismasi na kumuacha mtoto niliyemzaa na mwanamume mwingine kabla ya kuolewa naye. Nifanyeje? Sio ubaguzi kwa mtoto wowote ndani ya ndoa ni jeraha kubwa linaloweza kuacha maumivu ya kudumu, hasa kwa mtoto asiye na hatia. Ni muhimu kuzungumza na mume wako kwa utulivu lakini kwa msimamo, umweleze wazi kuwa mtoto huyo ni sehemu ya familia na anahitaji kupendwa na kutunzwa kama wengine. Mama mkwe hanitaki miaka miwili baada ya kuoana na mwanawe Ni miaka miwili tangu tuoane na mume wangu, na pamoja tumejaliwa mtoto mmoja. Tangu mwanzoni mama mkwe alikuwa hanipendi, na nilidhani kwamba muda unavyoendelea kusonga, angebadilika. Lakini mambo ni yale yale. Hanipendi na hatokuja kunipenda. Naomba usahuri. Sio kila mama mkwe atakupenda, na hilo si kosa lako bali ni mipaka ya moyo wake. Kilicho muhimu ni kudumisha heshima bila kujishusha, kuepuka mashindano yasiyo na faida, na kuhakikisha mume wako anafahamu hali halisi ili asimame katikati kwa haki. Usilazimishe upendo usiotolewa kwa hiari; jenga ndoa yako, mleeni mtoto wenu kwa amani. Wazazi wamenitafutia mke mwingine, nitampendaje? Mama watoto wangu aliniacha miaka miwili iliyopita, suala lililoniachia majonzi mengi sana. Hata nilikuwa nimeanza kuingilia unywaji pombe. Sasa wazazi wangu wameamua kuniletea mke eti kuniondolea upweke. Je, nitaanzaje kumpenda mtu nisiyemjua? Maumivu ya kuachwa huleta pengo kubwa moyoni, na ni kweli wazazi wako wanatafuta kukuokoa dhidi ya upweke, lakini mapenzi hayaoti kwa amri. Huwezi kumpenda mtu mara moja, bali unaweza kumpa nafasi ya kumjua taratibu bila presha, huku ukiwa mkweli na nafsi yako kama bado hujapona kabisa. Kabla ya kufunga ndoa, hakikisha unajijenga kwanza kihisia, maana ndoa haipaswi kuwa dawa ya jeraha, bali safari ya watu wawili walio tayari.