Mahakama ya Rufaa nchini imefuta hukumu ya kifungo cha maisha jela aliyokuwa amehukumiwa Rahim Baksh Marabzay, baada ya kukiri kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini yenye uzito wa kilo 41.713 yenye thamani ya zaidi ya Sh2.085 bilioni.