Ruksa ACT-Wazalendo kupinga uteuzi wabunge viti maalumu

Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu Dodoma, imeridhia maombi ya Chama cha ACT–Wazalendo ya kufungua shauri la mapitio ya kimahakama kupinga uteuzi wa wabunge wa viti maalumu uliofanywa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).