Wakati zikiandaliwa kanuni kuwabana wawekezaji kuwajibika kwa jamii (CSR) katika maeneo wanayowekeza, Serikali imesema inatambua mchango wa sekta binafsi katika kukuza na kuendeleza uwekezaji, hivyo itahakikisha inaweka mazingira wezeshi kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.