Bei ya mchele Mbeya haishikiki, serikali yaingilia kati

Kutokana na kupanda kwa bei ya mchele na bidhaa nyingine jijini Mbeya, serikali wilayani humo imechukua hatua za haraka kuunda timu maalumu kufuatilia baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha kiholela bei hizo kwenye masoko.