Ujenzi wa viwanda vya nguo na dawa za binadamu katika eneo la viwanda Dunga Zuze, Mkoa wa Kusini Unguja, umetajwa kuwa suluhisho la kupunguza gharama za uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi na kuhakikisha upatikanaji wa haraka na wa bei nafuu kwa wananchi wa Zanzibar.