Uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Uzi–Ng’ambwa pamoja na barabara zake umeibua matumaini mapya kwa wakazi wa visiwa vya Uzi na Ng’ambwa, ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya usafiri kutokana na kutegemea maji ya bahari kupwa na kujaa ili kuingia na kutoka visiwani humo.