Serikali yatangaza kipaumbele cha ajira kwa vijana

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaweka kipaumbele katika utoaji wa ajira kwa vijana kwa kuhakikisha fursa zinazotokana na miradi ya maendeleo zinafika hadi ngazi ya shehia badala ya kubaki katika ofisi za mikoa na wilaya pekee.