Othman ataka Taifa lijengwe juu ya haki, Katiba 2026

Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, ametumia salamu za Mwaka Mpya 2026 kuwataka Watanzania kuutumia kama fursa ya kuliponya Taifa, kurejesha misingi ya Katiba na kujenga umoja wa kitaifa unaotokana na haki, uwajibikaji na ridhaa ya wananchi.