Wananchi wamvaa mbunge ubovu wa barabara, wataka ufumbuzi Mbeya Vijijini
Wananchi wa kata za Itewe, Igoma na Ulenje, Wilaya ya Mbeya Vijijini, wamemwomba Mbunge wao, Patali Shida, kuingilia kati changamoto ya ubovu wa barabara wakisema imekuwa kikwazo kwa shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii.