Siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti kupanda kwa bei ya bidhaa jijini Mbeya, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Solomon Itunda, imefanya ziara ya kushtukiza katika baadhi ya maduka na kuwahakikishia wananchi kuwa hatua za kudhibiti hali hiyo zinachukuliwa.