Kanisa lawasogezea wananchi wa Tarakea huduma za afya

Kanisa la The Sowers Evangelical International Church limeanza ujenzi wa zahanati katika Kata ya Tarakea Motamburu, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, hatua inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa maeneo ya pembezoni na ya mpakani ya mji wa Tarakea.